Bei ya bidhaa mbalimbali za kimsingi katika soko la Makutano, kaunti ya Pokot Magharibi, imeendelea kuongezeka kwa kiwango kikubwa, hali ambayo imehusishwa na ukame mkali ulioshuhudiwa msimu huu pamoja na kupanda kwa bei za mafuta mwanzoni mwa mwaka huu.
Wakizungumza na Aperit Fm, baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wamesema kupanda kwa bei kumeendelea kuwaathiri pakubwa wenyeji wanaotegemea bidhaa hizo kwa matumizi ya kila siku.
Wafanyabiashara hao pia wanasema hali hiyo imewasababishia hasara, huku baadhi ya bidhaa zao zikiharibika kutokana na ukosefu wa soko la uhakika na changamoto zinazohusiana na hali ya hewa.
Wamewataka wadau husika kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hiyo ili kupunguza mzigo kwa wafanyabiashara na wananchi wanaotegemea bidhaa hizo za kimsingi.
Aidha wamelalamikia changamoto kama vile ukosefu wa mazingira safi ya kufanyia biashara inayohusisha uhaba wa vyoo na maji safi wakitaka hali hiyo kuangaziwa ili kupiga jeki kushughuli za kibiashara mjini humo na kuepesha mkurupuko wa magonjwa
APERIT FM,HII NI YETU

