You are currently viewing MATAMSHI YA WAZIRI MURKOMEN DHIDI YA SENETA MANDAGO NA KATIBU CHRIS KIPTOO YAKASHIFIWA VIKALI

MATAMSHI YA WAZIRI MURKOMEN DHIDI YA SENETA MANDAGO NA KATIBU CHRIS KIPTOO YAKASHIFIWA VIKALI

Mbunge wa kesses   CPA Julius Rutto amemsuta vikali waziri wa usalama    Kipchumba Murkomen kufuatia matamshi yake yaliyomkosoa seneta Jackson Mandago na katibu wa wizara ya fedha DR. Chris Kiptoo.

‎Rutto   amedai matamshi hayo ni mazito na yanahitaji uchunguzi ili kubaini maana na dhamira yake.

‎Aidha, Rutto amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kutumia lugha ya heshima na inayojenga umoja badala ya kutoa kauli zinazoweza kutafsiriwa kama vitisho au kuzua taharuki miongoni mwa wananchi.

Amesema tofauti za kisiasa zinapaswa kushughulikiwa kwa njia ya mazungumzo na kuheshimu misingi ya utawala wa sheria.