‘Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, hajafadhili kundi la linda mwananchi hata kwa peni moja’. Ni msimamo wa chama cha Jubilee kufuatia mashambulizi ambayo yameelekezwa kwake wikendi nzima, yakiongozwa na rais William Ruto na wandani wake kwamba Kenyatta ndiye mfadhili mkuu wa kundi hilo.
Naibu kongozi wa chama cha Jubilee Joseph Manje, amepuuzilia mbali madai hayo akisema Uhuru yuko kwenye harakati za kumkabidhi Fred Matiang’ uwongozi wa chama hicho ishara kwamba hana nia ya kushiriki siasa moja kwa moja.
Amefafanua kuwa, kando na ushauri wa hapa na pale kwa viongozi wa chama chake cha Jubilee na mrengo wa Azimio, haja husika katika ufadhili wa makundi mengine, kama linda mwananchi kama inavyo daiwa na viongozi hao serikalini.
Kwenye mahojiano Manje ameshangazwa na mapendekezo ya baadhi ya viongozi serikalini, kwamba Uhuru apokonywe marupurupu yake ya kustaafu kwa madai kwamba anajihusisha na siasa ya miegemeo licha ya kustaafu.
Ikumbukwe wikendi hii iliyokamilika, rai Ruto aliongoza mashambulizi hayo kwenye mikutano mbalimbali, akimtaja Uhuru kuwa bwenyenye ambaye anatoa hela za kufadhili na kupiga jeki shughuli za linda mwananchi na upinzani kwa ujumla.
APERIT FM, HII NI YETU

