You are currently viewing MSWADA WA MAKOSA YA KINGONO MWAKA WA 2026 LIMEIDHINISHA NA NCAJ.

MSWADA WA MAKOSA YA KINGONO MWAKA WA 2026 LIMEIDHINISHA NA NCAJ.

Baraza la kitaifa la usimamizi wa haki nchini NCAJ, limeidhinisha mswada wa makosa ya kingono mwaka wa 2026, hatua inayolenga kuimarisha sheria za kukabili ukatili wa kingono na kijinsia pamoja na kuboresha utoaji wa haki nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Akizungumza baada ya mkutano wa 38 wa baraza hilo, Jaji mkuu Martha Koome, amesema msawada huo utaimarisha namna nchi inavyo shughulikia makosa ya kingono yakiwamo yanayofanywa kupitia teknologia, mauaji ya wanawake pamoja na aina mpya za ukatili, uku ukiongeza ulinzi na huduma kwa manusura.

Baraza hilo pia limehusisha kamati maalum, ya maandalizi ya uchaguzi wa 2027, itakayoongozwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC Erastus Ethokon, hili kuimarisha uratibu wa taasisi za haki, katika kushughulikia migogoro ya uchaguzi, na kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani na wakuaminika.

Kwa upande wake mkuu wa mashtaka ya umma DPP Renson Mulele Ingonga, amewonya viongozi wa kisiasa wanaotumia wahuni kuzua vurugu akisisitiza kuwa watakabiliwa kisheria bila kujali hadhi yao ya kisiasa.

                                                                                     APERIT FM HII NI YETU