You are currently viewing NYORO KAFANYA UWAMUZI BINAFSI

NYORO KAFANYA UWAMUZI BINAFSI

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ametangaza rasmi kujiondoa katika chama cha UDA na kujiunga na upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Nyoro alitoa tangazo hilo jana usiku katika kikao na wanahabari jijini Nairobi. Akisema yeye pamoja na wafuasi wake wamejiunga na chama cha People’s Party of Kenya. Amesema uwamuzi huo umefikiwa baada ya mashauriano na tafakari, kuhusu mwelekeo wa kisiasa unaofaa zaidi kwa wakenya kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Kulingana na Nyoro, katika kipindi hicho alizungumza na viongozi kadhaa wa upinzani wakiwamo aliyekwa naibu wa rais Rigathi Gachagua, kiongozi wa chama cha PLP Martha Karua, waliokuwa mawaziri Peter Munya na Fred Matiang, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, pamoja na gavana wa Siaya James Orengo.

Amesema uzoefu wake serikalini, ulimpa nafasi ya kutathmini hali ya nchi katika sekta mbalimbali, na kubainisha sekta zinazoitaji mabadiliko.

Mbunge huyo wa Kiharu, aidha ametangaza kuanza ziara za kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini akitaja Uasin Gishu, Kericho na Nandi pamoja na Bonde la Ufa kwa ujumla, kuwa miongoni mwa maeneo atakayo yatembelea.

Amesema ziara hizo zitampa fursa ya kuzungumza na wakenya kuhusu utendaji wa serikali walio ichagua mwaka wa 2022.

Katika uchaguzi mkuu wa 2022, Ndindi Nyoro alichaguliwa kwa tiketi ya UDA na alikuwa mmoja wa viongozi waliokuwa na ushawishi mkubwa katika serikali ya kenya kwanza.

                                                                                                                             APERIT FM, HII NI YETU