Serikali imezindua rasmi kaunti ndogo ya Kolowa wakati wa ziara ya tathmini ya hali ya usalama katika Bonde la Kerio.
Shughuli hiyo iliongozwa na waziri wa usalama Kipchumba Murkomen ,viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na maafisa wa usalama, ambao walifanya tathmini ya hali ya usalama katika eneo hilo na kujadiliana na wananchi kuhusu hatua zinazochukuliwa kuimarisha amani na usalama.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi huo, viongozi walieleza kuwa kuanzishwa kwa kaunti ndogo ya kolowa kutarahisisha utoaji wa huduma za serikali, kuimarisha uratibu wa shughuli za kiusalama, na kuleta maendeleo karibu zaidi na wananchi.
Waliwahimiza wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa kuhusu vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na usalama, huku serikali ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha ukanda wa kerio unakuwa salama na wenye mazingira bora kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Uzinduzi wa kaunti ndogo ya Kolowa unatarajiwa kuongeza ufanisi wa utawala, kuimarisha usalama, na kuboresha utoaji wa huduma za umma katika eneo hilo.
