You are currently viewing TUTACHUKUA HATUA ZA KISHERIA KUPINGA MPANGO WA UPANUZI WA UWANJA WA KIPCHOGE

TUTACHUKUA HATUA ZA KISHERIA KUPINGA MPANGO WA UPANUZI WA UWANJA WA KIPCHOGE

Kiongozi wa wachache katika Bunge la Kaunti ya Uasin Gishu na Mwakilishi wa Langas, Francis Muya, ametishia kuchukua hatua za kisheria kupinga mpango wa upanuzi wa Uwanja wa Kipchoge Keino kuelekea eneo la makaburi.

‎Muya anaitaka serikali ya kaunti kueleza kwa nini shughuli za ujenzi na uchimbaji zilianza katika eneo hilo bila kuwahusisha kikamilifu familia zilizo na wapendwa wao waliozikwa katika makaburi hayo. Familia zimeeleza wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa miili kuhamishwa ili kutoa nafasi kwa mradi wa uwanja.

‎  Amedai   kuwa serikali ya kaunti ilipaswa kufuata taratibu zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na kuwahusisha wananchi kupitia mchakato wa ushirikishwaji wa umma pamoja na Bunge la Kaunti, kabla ya kuchukua hatua zozote zinazoweza kuathiri eneo la makaburi.

‎Muya ameitaka serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu kuingilia kati na kusitisha shughuli zinazoweza kuathiri makaburi hadi familia na jamii zitakapopewa maelezo ya kutosha kuhusu mipango ya upanuzi wa uwanja.