You are currently viewing VIJANA WABUNI VUGUVUGU LA KUHAMASISHA AMANI CHERANGANY

VIJANA WABUNI VUGUVUGU LA KUHAMASISHA AMANI CHERANGANY

Vijana kutoka eneo bunge la  Cherang’any   wameanzisha vuguvugu la kuhamasisha uwezeshaji wa kiuchumi na kudumisha amani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao

Kampeni hiyo inalenga kuwahimiza vijana kujihusisha na shughuli za kujikwamua kiuchumi, huku wakijiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani kama ukabila, uhalifu, matumizi ya dawa za kulevya na vurugu za kisiasa.

Viongozi wa vuguvugu hilo wamesema mshikamano wa jamii ni muhimu katika kipindi hiki cha uchaguzi, ili kuhakikisha mchakato  huo unafanyika kwa utulivu na bila migawanyiko.