Maelfu ya watu wanaendelea kumiminika katika eneo la Cheparor, Kaunti ya West Pokot, kufuatia taarifa za ugunduzi wa dhahabu.
Kwa mujibu wa taarifa watu kutoka maeneo mbalimbali wamewasili katika eneo hilo wakitafuta fursa ya kupata madini hayo, baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba wakazi wa eneo hilo waligundua dalili za dhahabu.
Haya yanajiri wakati ambapo Wataalamu wanasisitiza umuhimu wa uchunguzi wa kisayansi na vipimo vya kimaabara kabla ya kuthibitisha ukubwa na thamani ya madini hayo.
Hata hivyo wakazi wanaotembelea eneo hilo wanahimizwa kufuata maagizo ya mamlaka na kuepuka shughuli za uchimbaji katika maeneo yasiyo salama, huku serikali ikitarajiwa kutoa tathmini rasmi kuhusu madai ya ugunduzi huo.

