You are currently viewing WAKAAZI WA POKOT MAGHARIBI WATAKA VIONGOZI KUACHA SIASA ZA MIRENGO YA ‘5G’ NA ‘MESSAGE’

WAKAAZI WA POKOT MAGHARIBI WATAKA VIONGOZI KUACHA SIASA ZA MIRENGO YA ‘5G’ NA ‘MESSAGE’

Wakaazi katika kaunti ya Pokot Magharibi, wametoa wito kwa viongozi kuweka kando tofauti zao kisiasa hasa kauli mbiu za massage na 5g ambazo ni mirengo za kisiasa katika kaunti hiyo na kuwatumikia wananchi ipasavyo.

Wakizungumza na Aperit fm, wanasema viongozi hawawajibikii kazi zao bali wamezamia siasa za mirengo na kuwaacha wananchi bila maendeleo katika kaunti hiyo, huku wakiwataka viongozi kuiga mfano wa viongozi wenzao toka kaunti jirani za turkana na trans-nzoia na kuweka maslahi ya wapiga kura kipaumbele.

Wameendelea kusisitiza kuwa viongozi katika kaunti ya Pokot Magharibi wanafaa kupaza sauti ili maendeleo imfikie mwananchi, badala ya kauli mbiu za massage na 5g, licha ya vuguvugu zote kuwa ndani serikali ya kenya kwanza huku ukame wa maendeleo ukikithiri.

Wamesisitiza umoja na amani, na kuhakikisha miundo mbinu kama vile barabara, nyumba za bei nafuu, umeme mashinani mingoni mwa miradi mingine muhimu inamfikia mwananchi wa chini.