You are currently viewing WAMALWA ATOA WITO WA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO

WAMALWA ATOA WITO WA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI UJAO

Aliyekuwa mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa, ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wananchi kuhakikisha kampeni na uchaguzi wa mwaka 2027 unaendeshwa kwa amani.

Wamalwa amewahimiza viongozi kuepuka lugha ya uchochezi, vitisho na siasa za migawanyiko, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu misingi ya demokrasia na haki za wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.

Amesema tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa chanzo cha uhasama miongoni mwa wananchi, akitaka viongozi kushindana kwa sera, mipango ya maendeleo na hoja badala ya kuchochea migawanyiko.

Aidha  ametoa wito kwa vijana kutotumiwa na wanasiasa kuvuruga amani wakati wa kampeni  akisema ‎ amani ni msingi muhimu wa maendeleo na kwamba viongozi wote wana jukumu la kuhakikisha Kenya inafika katika uchaguzi mkuu wa 2027 ikiwa na utulivu na mshikamano wa kitaifa.