You are currently viewing WANAFUNZI NA WALIMU WAO WANAPOKEA MATIBABU BAADA YA AJALI MBAYA KABARNET.

WANAFUNZI NA WALIMU WAO WANAPOKEA MATIBABU BAADA YA AJALI MBAYA KABARNET.

Wanafunzi kadhaa na walimu wanaendelea kuhudumiwa hospitalini baada ya basi lao la shule kuhusika kwenye ajali katika barabara ya Kabarnet-Margat.

Kulingana na shirika la msaklaba mwekundu, basi hilo lilikuwa likiwasafirisha wanafunzi 56 na walimu 4 wakati ajali ilipotokea.

Basi hilo linalomilikiwa na shule ya upili ya mseto ya aic Lomut iliyoko kwenye kaunti ya Pokot Magharibi, lilipoteza mwelekeo lilipokuwa likipiga kona maarufu ya ‘SS’ uko Kabarnet. Wanafunzi hao walikuwa wakirudi shuleni baada ya ziara ya kielimu.

Katika taarifa shirika la msalaba mwekundu, limesema wanafunzi na walimu wote walio husika kwenye ajali hiyo, walipelekwa katika Hosipitali ya Rufaa ya Kaunti ya Baringo kwa ajili ya matibabu.

Shirika hilo la mslaba mekundu, limesema kwamba linaendelea kufatilia hali hiyo, uku uchunguzi ukianzishwa ili kubainisha chanzo cha ajali hiyo.