Waziri wa Jinsia na Utamaduni, Hannah Cheptumo, ametoa wito kwa wanawake wengi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Bi. Cheptumo amesema ushiriki wa wanawake katika siasa ni muhimu kwa kuimarisha uwakilishi wenye usawa na kuhakikisha sauti za wanawake zinasikika katika ngazi zote za maamuzi.
Aidha, amewahimiza wakenya kuwapa wanawake nafasi ya kuongoza kwa kuwachagua kulingana na uwezo, uadilifu na sera zao, akisema wanawake wameonyesha uwezo mkubwa kwenye maswala ya uongozi katika sekta mbalimbali.
Amesisitiza kuwa kuongezeka kwa idadi ya wanawake katika nafasi za kisiasa kutachangia maendeleo ya jamii, kuimarisha usawa wa kijinsia na kuendeleza ajenda ya maendeleo jumuishi nchini kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027.

