Mbunge wa Baringo Kusini, Charles Kamuren, amesema kuwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa Ol-Kalou yanapaswa kuwa funzo kwa viongozi wanaomuunga mkono Rais William Ruto.
Amesema kuwa kushindwa huko kulitokana na kile alichokitaja kuwa majigambo ya baadhi ya viongozi, badala ya kusikiliza sauti na mahitaji ya wananchi.
Kamuren amewataka viongozi wa kisiasa kujenga uhusiano mzuri na wapiga kura ili kuimarisha uungwaji mkono kwa serikali.
Ameonya kuwa baadhi ya viongozi wanaodai kumuunga mkono rais ruto wanaendelea kuharibu taswira yake kwa matamshi na mienendo yao, akiwataka wajikite katika kuwatumikia wananchi badala ya siasa za majigambo.

