You are currently viewing UEFA YASEMA UONGOZI WA FIFA UMEPOTEZA IMANI

UEFA YASEMA UONGOZI WA FIFA UMEPOTEZA IMANI

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), Gianni Infantino, amesema shirikisho hilo limefuta mpango wake wa kuuza sehemu ya umiliki wa mashindano ya Kombe la Dunia kwa wawekezaji wa kibinafsi.

Kufuatia tangazo hilo, Shirikisho la soka Ulaya, UEFA limepongeza uamuzi huo wa FIFA lakini likasema uongozi wa sasa wa FIFA haujapoteza tu imani ya UEFA, bali pia ya wanachama wengine wengi wa familia ya soka duniani.

Limesema litaanza mara moja kushirikiana na washirika na wadau duniani kote pamoja na sekta nzima ya soka ili kupendekeza njia mpya ya kusambaza rasilimali kupitia mpango uliopo wa FIFA Forward.

UEFA pia imesema ushindi huo ni wa sekta nzima ya soka, na akaongeza kuwa pendekezo hilo limeondolewa, lakini kazi ya kurejesha imani kwa FIFA ndiyo imeanza.

                                                                                                                                  APERIT FM, HII NI YETU