You are currently viewing IEBC KWENYE MIZANI

IEBC KWENYE MIZANI

Mswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2024, umeibua mjadala mpya, baada ya kupendekeza kuondolewa kwa sharti la kisheria, linaloitaka tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kutangaza moja kwa moja matokeo ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura.

Mswada huo ambao uliidhinishwa na seneti mwezi Disemba 2024, na sasa unasuburi kujadiliwa na bunge la kitaifa, unapendekeza kufutwa kwa kifungu cha 39 cha sheria ya uchaguzi, na kuwekwa masharti mapya yasiyo lazimisha IEBC kuendesha matangazo ya moja kwa moja ya matokeo, yanapotangazwa katika vituo vya kupigia kura.

Wanaopinga pendekezo hilo wanasema hatua hiyo inaweza kupunguza uwazi wakatika shughuli ya kuhesabu kura na kudhoofisha imani ya wananchi kuhusu uwaminifu wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kwa mujibu wa mswada huo unaoungwa mkono na serikali, IEBC itaendelea kutangaza na kusimamia matokeo ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria, lakini haitakuwa tena na wajibu wa kisheria wa kuwezesha matangazo ya moja kwa moja ya matokeo, yakiwamo ya uchaguzi wa urais kutoka katika vituo vya kupigia kura.

Pendekezo hilo linatarajiwa kuwa miongoni mwa maswala yatakayo zua mjadala mkali, katika bunge la kitaifa.

                                                      APERIT FM, HII NI YETU