Gavana wa kaunti ya Elgeyo Marakwet, Wisley Rotich, amemrai Rais William Ruto kuhudhuria hafla rasmi ya ufunguzi wa uwanja wa Kamariny siku moja kabla ya maadhimisho ya sherehe za mashujaa yatakayofanyika katika kaunti ya Uasin Gishu.
Gavana Rotich amesema uwepo wa Rais katika hafla hiyo utakuwa ishara ya kutambua juhudi zilizowekwa katika kukamilisha uwanja huo, ambao unatarajiwa kuwa kichocheo cha kukuza vipaji vya michezo, hususan riadha, katika eneo la bonde la ufa na nchini kwa ujumla. Ameelezea matumaini kwamba uzinduzi huo utafungua ukurasa mpya wa maendeleo ya sekta ya michezo katika kaunti ya Elgeyo Marakwet

