Wakulima nchini wamehimizwa kutumia vyema musimu ujao wa mvua za Vuli za Septemba hadi Disemba mwaka huu, kupanda mbegu zilizoidhinishwa zinazo komaa mapema, na zinazo stahimili mabadiliko ya tabianchi.
Wito huo umetolewa huku Kenya ikitarajiwa kupata mavuno yaliyo chini ya kiwango cha kawaida mwaka huu, kutokana na ukame wa muda mrefu na mvua duni, iliyosababisha kushindwa kwa mimea katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei amesema mabadiliko ya tabianchi, yameathiri pakubwa uzalishaji wa chakula, lakini Kenya bado inauwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha, iwapo wakulima watatumia mbegu bora, teknologia zinazofaa na kupanda kwa wakati.
Koskei amesema serikali inaendelea kuchukua hatua za kuwalinda wakulima na walaji, kutokana na athari za kupungua kwa uzalishaji wa kilimo.
Ikumbukwe idara ya utabiri wa hali ya anga imetabiri kuwa mwezi Agosti utakuwa na hali ya ukavu katika sehemu kubwa ya nchi, ku joto likitarajiwa kuwa juu ya wastani na kuondoa unyevu-unyevu kwenye udongo.
Maamlaka ya kitaifa ya kudhibiti ukame NDMA imesema hali ya ukame inazidi kuwa mbaya katika baadhi ya kaunti kame na nusu kame, hali ambayo imeathiri malisho, vyanzo vya maji na usalama wa chakula.
Wakulima pia wamehimizwa kuvuna, kukausha na kuifadhi vizuri mazao yaliyo komaa, uku wafugaji nao wakitakiwa kuhakikisha mifugo wanapata maji ya kutosha, lishe ya ziada pale malisho yanapokuwa haba, na ulinzi dhidi ya vipindi vya baridi na joto kali.
APERIT M, HII NI YETU

