You are currently viewing UGUNDUZI WA DHAHABU KANYARKWAT KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAIBU MSISIMKO MIONGONI MWA WAKAAZI

UGUNDUZI WA DHAHABU KANYARKWAT KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAIBU MSISIMKO MIONGONI MWA WAKAAZI

Maelfu ya watu wanaendelea kumiminika katika eneo la Cheparor, Kaunti ya West Pokot, kufuatia taarifa za ugunduzi  wa dhahabu.

Kwa mujibu wa taarifa   watu kutoka maeneo mbalimbali wamewasili katika eneo hilo wakitafuta fursa ya kupata madini hayo, baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba wakazi wa eneo hilo waligundua dalili za dhahabu.

 Haya yanajiri wakati ambapo Wataalamu wanasisitiza umuhimu wa uchunguzi wa kisayansi na vipimo vya kimaabara kabla ya kuthibitisha ukubwa na thamani ya madini hayo.

Hata hivyo ‎wakazi   wanaotembelea eneo hilo wanahimizwa kufuata maagizo ya mamlaka na kuepuka shughuli za uchimbaji katika maeneo yasiyo salama, huku serikali ikitarajiwa kutoa tathmini rasmi kuhusu madai ya ugunduzi huo.