Mbunge wa Marakwet Magharibi, Timothy Toroitich, amesema ameiweka eneo bunge hilo kwenye ramani ya kenya kupitia miradi na maendeleo aliyotekeleza wakati wa uongozi wake.
Akizungumza na wakazi wa Kapcherop, Toroitich ameangazia rekodi yake ya utendakazi na kusema amejitahidi kuhakikisha mahitaji ya wananchi yanafanyiwa kazi.
Mbunge huyo amewataka wakazi wa Kapcherop kuendelea kumpa uungwaji mkono katika uchaguzi ujao ili apate nafasi ya kuendeleza mipango yake ya maendeleo katika Marakwet West.
Toroitich amesema ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kuhakikisha miradi iliyoanzishwa inaendelea na mipango mingine inatekelezwa kwa manufaa ya wakazi.
Ameongeza kuwa anajivunia mchango wake katika kuinua hadhi ya marakwet west kitaifa na kuifanya eneo hilo kutambulika zaidi kupitia shughuli za maendeleo na uongozi.
APERIT FM,HII NI YETU

