Baraza la wazee wa jamii ya Pokot limeelezea kutamaushwa na kisa cha uvamizi na wizi wa mifugo katika eneo la Ombolion Pokot Kaskazini, swala wanalodai linachangiwa na kuwepo kwa silaha haramu miongoni mwa wakaazi wa kaunti jirani ya turkana.
Baraza hilo likiongozwa na Mastait Lokiles linasema silaha haramu zilizoko mikononi mwa raia katika kaunti jirani ya Turkana imepelekea kuzuka tena uvamizi huo licha ya idara ya usalama na viongozi kushinikiza usalimishaji wa silaha hizo kaskazini mwa bonde la ufa.
Anasema baraza la wazee wa jamii ya Pokot wanaunga mkono oparesheni ya serikali kutwaa bunduki japo mpango huo unapaswa kutekelezwa kwa usawa katika kaunti zote zinazoshuhudia uhalifu.

