You are currently viewing SOKO LA NGINYANG LAFUNGULIWA TENA BAADA YA KUFUNGWA KWA MUDA

SOKO LA NGINYANG LAFUNGULIWA TENA BAADA YA KUFUNGWA KWA MUDA

Wakazi wa Tiaty wamekaribisha kufunguliwa tena kwa soko la mifugo la Nginyang’, kufuatia kuimarika kwa usalama katika eneo hilo.

Hatua hiyo inafuatia operesheni ya kijasusi iliyolenga kuondoa silaha zinazomilikiwa   na raia kinyume cha sheria.

Wametaja soko hilo   miongoni mwa zile   zinazojulikana kwa biashara ya mbuzi bora, japo lilifungwa kutokana na ukosefu wa usalama pamoja na wasiwasi kuhusu biashara ya mifugo iliyoibwa.

Kulingana nao kufungwa kwa soko hilo lilikuwa pigo kubwa kwa wafanyabiashara na wakazi wanaotegemea ufugaji na biashara ya mifugo kama chanzo cha mapato.

Wakazi sasa wanatumai kuwa kurejea kwa shughuli za soko kutafufua biashara na kuboresha maisha ya jamii inayotegemea mifugo kwa kujipatia riziki.

APERIT FM,HII NI YETU