You are currently viewing NYORO AMETAKA UPINZANI KUUNGANA ILI KUPATA NAFASI BORA YA KUMNG’ATUA MADARAKANI RAIS RUTO

NYORO AMETAKA UPINZANI KUUNGANA ILI KUPATA NAFASI BORA YA KUMNG’ATUA MADARAKANI RAIS RUTO

Kinara wa chama cha Kenya People’s Party ambaye pia ni Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, amesema viongozi wa upinzani wanapaswa kuweka kando maslahi yao ya kibinafsi na kuungana ikiwa wanataka kufanikisha azma ya kumng’oa Rais William Ruto madarakani katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika eneo la Wotee kaunti ya Makueni , Ndindi Nyoro amesema umoja wa viongozi wa upinzani ni muhimu katika kujenga nguvu moja ya kisiasa inayoweza kukabiliana na serikali iliyopo madarakani.

Amesema viongozi hao wanapaswa kuangalia maslahi ya wakenya na kuweka mbele ajenda ya pamoja badala ya tofauti zao binafsi.

Kauli ya nyoro inajiri huku maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao yakianza kuchukua sura katika maeneo mbalimbali nchini.

APERIT FM,HII NI YETU