You are currently viewing RAEL ALEUTUM AORODHESHWA WA PILI BORA KATI YA WAWAKILISHI WA KIKE NCHINI

RAEL ALEUTUM AORODHESHWA WA PILI BORA KATI YA WAWAKILISHI WA KIKE NCHINI

Mwakilishi wa akina mama katika kaunti ya pokot maghaibi , rael kasiwai aleutum, ameshabikia taarifa za utafiti wa infotrak zilizomtaja kuwa mbunge wa kike wa pili nchini kwa utendaji bora.
Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, aleutum amewapongeza wakazi wa west pokot kwa imani na ushirikiano wao, akisema mafanikio hayo ni ya wananchi wote wa kaunti hiyo.
Amesisitiza kuwa kutambuliwa huko kutamtia nguvu ya kuongeza bidii katika kutekeleza majukumu yake ya uwakilishi, kusimamia maendeleo, na kutetea maslahi ya wananchi
Aleutum ameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha huduma bora na maendeleo endelevu yanawafikia wananchi wote wa west pokot.

Kwa upande wa maseneta Kamau Murango wa Kirinyaga ametajwa kuongoza orodha hiyo kwa asilimia 69,akifuatwa na John Methu wa Nyandarua kwa asilimia 68,John Nyutu wa Murang’a,Samson Cherargei wa Nandi,Aaron Cheruiyot wa Kericho,Vincent Chemitei wa Baringo,Richard Onyonka wa Kisii, Dan Maanzo wa Makueni,Edwin Sifuna wa Nairobi,Steve Lelegwe wa Samburu,Ali Roba Mandera,Enoch Wambua Kitui,Julius Murgor wa Pokot Magharibi Hillary Sigei wa Bomet na Jackson Mandago wa Uasin Gishu.