You are currently viewing KAMATI YA BUNGE KUHUSU HAZINA YA MAENDELEO YA MAENEO BUNGE NG-CDF YATOA RATIBA YA USAMBAZAJI WA FEDHA HIZO KWENYE MAENEO BUNGE YOTE 290 NCHINI

KAMATI YA BUNGE KUHUSU HAZINA YA MAENDELEO YA MAENEO BUNGE NG-CDF YATOA RATIBA YA USAMBAZAJI WA FEDHA HIZO KWENYE MAENEO BUNGE YOTE 290 NCHINI

Mbunge wa Eldama Ravine na Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hazina ya maendeleo ya maeneo bunge (NG-CDF), Musa Sirma, amewasilisha rasmi bungeni ratiba ya mgao wa fedha kuelekezwa kwenye maeneo bunge 290 nchini kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027.

‎Ratiba hiyo inalenga kuwezesha upangaji wa bajeti na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ngazi ya maeneo bunge ili kusaidia kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi na ukarabati wa shule, utoaji wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi, maendeleo ya miundombinu pamoja na miradi mingine ya kijamii inayoboresha maisha ya wananchi.

‎Sirma ameeleza kuwa viwango vya mgao vinazingatia mfumo uliowekwa kisheria, unaozingatia mahitaji ya maendeleo pamoja na vigezo vinavyotumika katika ugavi wa rasilimali na kuleta tija kwenye jamii