You are currently viewing ONYO KWA WAMILIKI WA SILAHA HARAMU KASKAZINI MWA BONDE LA UFA

ONYO KWA WAMILIKI WA SILAHA HARAMU KASKAZINI MWA BONDE LA UFA

Waziri wa usalama wa ndani ya Nchi Kipchumba Murkomen, ametoa onyo kali kwa majangili na wezi wa mifugo katika eneo la kasikazini mwa bonde la ufa, akisema serikali imehimarisha oparesheni maalum za kiusalama ili kukomesha uhalifu huo.

Akizungumza uko Ledero katika kaunti ya Samburu, Murkomen amesema oparesheni izo zinazoongozwa na taarifa za kijasusi, zinalenga kukusanya silaha haramu zinazomilikiwa na raia, kuvunja mitandao ya biashara haramu ya risasi na kudhibiti wizi wa mifugo.

Kulingana na waziri Murkomen, Serikali haitelegeza kamba katika vita dhidi ya wizi wa mifugo, ujangili na uhalifu mwingine.