You are currently viewing GAVANA NATEMBEYA AKIRI KUWA RAIS RUTO BADO ANA UUNGWAJI MKONO MKUBWA HAPA NCHINI

GAVANA NATEMBEYA AKIRI KUWA RAIS RUTO BADO ANA UUNGWAJI MKONO MKUBWA HAPA NCHINI

Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya amesema jamii ya Kalenjin inaendelea kumuunga mkono Rais William Samoei Ruto katika azma yake ya kutafuta muhula wa pili wa uongozi.

‎Natembeya ametoa kauli hiyo kwa namna ya ucheshi, akitambua kuwa licha ya mijadala na tofauti za kisiasa nchini, Rais Ruto bado ana uungwaji mkono mkubwa katika baadhi ya maeneo ya jamii ya Kalenjin.  

‎Gavana huyo pia amerejelea suala la kuondolewa kwa watu katika eneo la Msitu wa Mau, akisema hatua hiyo imekuwa na manufaa ya kisiasa kwa Rais Ruto. Natembeya amekumbusha kuwa wakati wa utekelezaji wa operesheni hizo, kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu ulinzi wa mazingira, makazi ya watu na masuala ya kisiasa yaliyohusishwa na Mau Forest.