Rais William Ruto leo anaongoza hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote East Africa Refinery, katika kaunti ya Lamu.
Mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Dangote Group kwa ushirikiano na Africa Finance Corporation, unakadiriwa kugharimu takriban dola bilioni 16, sawa na zaidi ya shilingi trilioni mbili za Kenya, Kikiwa na uwezo wa kusafisha mapipa laki saba ya mafuta ghafi kwa siku, na kukamilika ifikapo mwaka 2030.
Mradi huo unalenga kuongeza uwezo wa Afrika Mashariki wa kusafisha mafuta na kupunguza utegemezi wa bidhaa za mafuta zinazoagizwa kutoka nje, ukitarajiwa kuchochea maendeleo ya viwanda vinavyohusiana na mafuta, kemikali na mbolea Kwa mujibu wa taarifa , mafuta ghafi yatapatikana kutoka vyanzo vya ndani na nchi nyingine za Afrika Mashariki, huku uzalishaji ukilenga kuhudumia soko la Kenya pamoja na masoko ya kikanda.
Serikali inatarajia mradi huo kuimarisha usalama wa nishati, kuongeza shughuli za kiuchumi na kutoa nafasi za ajira moja kwa moja na kwa njia isiyo rasmi kwa mamia ya vijana
Hata hivyo, mradi huo unakabiliwa na changamoto za kisheria kuhusu ardhi inayopendekezwa kujengwa kiwanda hicho,Wakazi wakiwasilisha kesi wakipinga umiliki na matumizi ya ardhi hiyo
APERIT FM,HII NI YETU

