Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, amesema serikali inaimarisha vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya kwa kulenga mali na miundombinu inayotumiwa au kupatikana kutokana na biashara hiyo.
Akizungumza jijini Mombasa Murkomen amesema mali zote zitakazobainika kutumika katika biashara ya dawa za kulevya, au kununuliwa kutokana na mapato ya biashara hiyo, zitachukuliwa kama mapato ya uhalifu
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuzima mitandao ya biashara ya dawa za kulevya kwa kuwalenga sio tu wasafirishaji na wauzaji, bali pia wafadhili na mali zinazotumika kuwezesha biashara hiyo.
Wakati huo uo Murkomen amesema maafisa watakaobainika kusaidia, kuwezesha au kushirikiana na mitandao ya biashara haramu ya dawa za kulevya watakabiliwa na hatua kali za kinidhamu na za jinai.
Murkomen amesisitiza kuwa serikali inalenga kuvuruga mitandao ya biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafuatilia wafanyabiashara, wasafirishaji, wafadhili pamoja na wale wanaowasaidia kuendesha shughuli hizo.
APERIT FM,HII NI YETU

