You are currently viewing NAIBU RAIS ATOA HAKIKISHO LA KUIMARISHWA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA YA EL NINO BAADAYE MWAKA HUU

NAIBU RAIS ATOA HAKIKISHO LA KUIMARISHWA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA YA EL NINO BAADAYE MWAKA HUU

Naibu rais Profesa Kithure Kindiki amewahakikishia wakenya kuwa serikali imejipanga kikamilifu kukabiliana na athari za mvua ya El Niño zinazotarajiwa kunyesha nchini, huku akiwataka wananchi kutokuwa na hofu.

‎Akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya baraza la mawaziri, Profesa Kindiki amesema serikali imeweka mikakati ya mapema ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.

Kindiki pia amesema serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa usimamizi wa majanga kupitia sheria mpya inayolenga kuboresha uratibu wa shughuli za kukabiliana na majanga nchini.

Wakati huo uo, amezihimiza serikali za kaunti kuunda na kuanzisha timu za dharura za kukabiliana na majanga katika maeneo yao ili kuhakikisha mwitikio wa haraka endapo kutatokea maafuriko au dharura nyingine zinazohusiana na mvua za el niño.

‎Naibu Rais amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa, serikali za kaunti, mashirika ya uokoaji na wananchi ni muhimu katika kupunguza athari za majanga na kulinda maisha pamoja na mali za wakenya.