Watabiri wa hali ya hewa wameonya kuhusu uwezekano wa mvua kubwa katika kipindi cha oktoba hadi desemba mwaka huu, huku hali ya el niño ikitarajiwa kuchangia mabadiliko ya mifumo ya mvua katika eneo la afrika mashariki.
Shirika la Utabiri wa hali ya hewa duniani, limeripoti uwezekano mkubwa wa kutokea kwa El Niño mwaka 2026, hali ambayo inaweza kuathiri mifumo ya mvua katika eneo la pembe ya Afrika, ikiwemo Kenya.
Kwa mujibu wa wataalamu, ongezeko la mvua linaweza kusababisha hatari ya mafuriko, maporomoko ya ardhi na uharibifu wa miundombinu, hasa katika maeneo yaliyo hatarini.
Wakulima wametakiwa kufuatilia kwa karibu taarifa rasmi za hali ya hewa na kuchukua tahadhari mapema vilevile kutumia taarifa za utabiri wa hali ya hewa katika kupanga shughuli zao za kilimo, huku jamii zinazoishi karibu na mito na maeneo ya mabonde zikitakiwa kuwa waangalifu kutokana na uwezekano wa kuongezeka kwa maji.

