Mbunge wa Loima, Protus Akujah, ameitaka kamati ya idara ya uchukuzi na miundombinu bungeni kueleza sababu za kutokuwepo kwa huduma za mamlaka ya kitaifa ya uchukuzi na usalama(NTSA), katika kaunti ya Turkana.
Akizungumza kwenye kikao cha bunge, Akujah, ameeleza kuwa mamlaka hiyo lina jukumu la kuhakikisha wakenya wote wananufaika na huduma zake, huku akiongeza kuwa licha ya kaunti hiyo kuwa miongoni mwa kaunti kubwa nchini, wakaazi wanalazimika kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma hizo jijini Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu, jambo ambalo amesema linawapa wenyeji wa gatuzi hilo mzigo wa gharama ya kupata huduma hizo.
Aidha, mbunge huyo amesema hatua hiyo inakandamiza sheria ya katiba inayopendekeza wakenya wote kupokea huduma hizo, na kutaka hatua za dharura kuchukuliwa ili kutoa fursa kwa wakaazi wa Turkana kunufaika na huduma za NTSA, katika hatua inayolenga kusaidia kuthibiti visa vya ajali na uvunjanji sheria barabarani.