Seneta mteule Margaret Kamar ameitaka serikali kuchukua hatua kudhibiti gharama ya juu ya chakula cha mifugo, akisema bei hizo zinaendelea kuwa mzigo kwa wafugaji na wakulima nchini.
Akizungumza bungeni Kamar amehoji vikwazo vinavyowazuia wakulima kuzalisha mahindi ya njano ambayo hutumika kama malighafi katika utengenezaji wa chakula cha mifugo.
Amesema kuna haja ya serikali kupitia upya sera zinazohusu uzalishaji wa mazao yanayotumika kutengeneza chakula cha mifugo, ili kuongeza uzalishaji wa ndani na kupunguza gharama.
Aidha, Kamar ameibua wasiwasi kuhusu ukosefu wa usindikaji wa soya nchini, akisema hali hiyo inawalazimisha wakulima na wazalishaji kutegemea uagizaji kutoka taifa la Uganda. Ametaka serikali kuweka mazingira yatakayochochea uzalishaji na usindikaji wa malighafi hizo nchini, hatua ambayo inaweza kupunguza utegemezi wa uagizaji na kusaidia kushusha gharama ya chakula cha mifugo
APERIT FM,HII NI YETU

