Rais William Ruto ameendelea kupigia debe ajenda yake ya kisiasa na kuwataka viongozi wa upinzani kujipanga na kuwa na sera na ajenda ya kueleweka kwa wananchi.
Akizungumza katika kaunti ya Kajiado Rais Ruto amesema upinzani unapaswa kuacha siasa za malalamishi na badala yake kuwasilisha mipango na sera zinazolenga kuboresha maisha ya wakenya.
Rais amesema serikali yake itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na mipango inayolenga kuboresha uchumi, kuongeza nafasi za ajira na kuimarisha huduma za kijamii.
Kiongozi wa taifa amewataka wananchi kuunga mkono mipango ya serikali yake, huku akiwasisitizia wapinzani umuhimu wa kuwa na ajenda mbadala yenye suluhu kwa changamoto zinazowakabili wananchi.

