Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua ameitaka mahakama kuzingatia matamshi yaliyotolewa na mbunge wa Suna Mashariki Junet Muhhamed na mbunge wa Lang’ata Felix Oduor maarufu kama Jalas, kuhusu madai ya matumizi ya hongo wakati wa mchakato wa kuondolewa kwa Gachagua madarakani.
Akizungumza nyumbani kwake Wamunyoro kaunti ya Nyeri, Gachagua amesema kauli za wabunge hao zinapaswa kutathiminiwa kwa uzito na majaji wanao sikiliza kesi zinazo husiana na kuondolewa kwake madarakani.
Gachagua amesema Junet na Jalas, wamekiri adharani kuwa baadhi ya wabunge, walipokea hongo ili kuunga mkono hoja ya kumwondoa ofisini.
Gachagua aidha amewataka viongozi wanao wania nyadhifa mbalimbali za uwongozi kupitia chama cha DCP na wafuasi wake kuepuka vurugu wakati wa mikutano ya kisiasa na badala yake kushindana kwa amani katika uchaguzi wa mchujo wa chama pamoja na uchaguzi mkuu wa 2027.
Kulingana na gachagua ameridhishwa na hali ya utulivu iliyo shuhudiwa wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou, na akiwataka wanachama wa DCP kuendeleza mshikimano huo uku ushindani wa nafasi mbalimbali za uwongozi ukiendelea.
Kauli hiyo imejiri baada ya gavana wa kaunti ya Nyandarua Kiarie Badilisha, kujiunga rasmi na chama cha DCP. Gachagua amesema gavana huyo na baadhi ya wawakilishi wadi wa kaunti ya Nyandarua, wamejitolea kutetea nyadhifa zao kupitia tiketi ya DCP katika uchaguzi wa 2027.
APERIT FM HII NI YETU

