You are currently viewing MAADHIMISHO YA SIKU YA MAAFISA WA UHIFADHI DUNIANI

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAAFISA WA UHIFADHI DUNIANI

Waziri wa utalii na wanyamapori Rebecca Miano, akiandamana na mkurugenzi mkuu wa shirika la kuifadhi wanyamapori nchini KWS Prof. Erastus Kenga, wameongoza taifa kwa maadhimisho ya siku ya maafisa wa uhifadhi duniani hii leo katika eneo la Mwakitau katika mbuga ya Tsavo Magharibi kwenye kaunti ya Taita Taveta.

Waziri Rebecca Miano akiwa na ujumbe wa rais William Ruto, amewapongeza maafisa hao akiwatambua kwa jina la ‘Green warrior’, kwamba wametekeleza wajibu muhimu katika kuhakikisha kwamba hifadhi za wanyapori zinasalia salama na kuifadhi rasilimali za taifa, kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Amesema kazi yao ambayo wamefanya imechangia pakubwa kwa ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia sekta ya utalii.

                                                                                                      APERIT FM, HII NI YETU