You are currently viewing WANAFUNZI WA GREDI YA 9 WATAANZA MCHAKATO WA KUCHAGUA SHULE ZA UPILI ZA NGAZI YA JUU YAANI SENIOR SCHOOL, KABLA YA KUJIUNGA NA GREDI YA KUMI

WANAFUNZI WA GREDI YA 9 WATAANZA MCHAKATO WA KUCHAGUA SHULE ZA UPILI ZA NGAZI YA JUU YAANI SENIOR SCHOOL, KABLA YA KUJIUNGA NA GREDI YA KUMI

Wizara ya elimu imetangaza kuwa wanafunzi wa gredi ya 9 wataanza mchakato wa kuchagua shule za upili za ngazi ya juu yaani Senior School, mkondo wa masomo Pathways na mchanganyiko wa masomo kuanzia Agosti 24 hadi Septemba 11 mwaka huu, kama sehemu ya maandalizi ya kujiunga na gredi ya 10 mwaka ujao.

Wizara hiyo ya elimu imesema shughuli hii ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mtaala wa umilisi CBC, ambapo wanafunzi watapata fursa ya kuchagua shule na mkondo wa masomo unao endeana na vipaji, uwezo na malengo yao ya baadae.

Mchakato uhuo utafanyika kwa mwongozo wa walimu, wazazi na washauri wa taaluma, ili kuhakikisha kila mwanafunzi anafanya uwamuzi unaofaa.

Kupitia mfumo wa CBC, wanafunzi watachagua miongoni mwa njia kuu za masomo ambazo ni Stem, yaani Sayansi, Teknoligia, Uhandisi na Hisabati, Sanaa na Michezo pamoja na Sayansi ya Jamii, kabla ya kuanza masomo ya gredi ya 10 mwaka ujao.

Wizara ya elimu imewahimiza wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika mchakato huo kwa kuwashauri na kuwaongoza wanafunzi, ili wachague masomo na taaluma zitakazo wawezesha kutimiza ndoto zao.