Mgombea wa chama cha DCP Sammy Douglas Kamau Waweru maarufu kama Ngotho, ametangaza mshindi wa uchaguzi wa ubunge wa eneo la Ol Kalou, kwenye kaunti ya Nyandarua, Kwa kupata kura 35, 440 kwa aslimi 83, na kumpiku mwenzake wa chama cha UDA Samuel Muchina, ambaye amepata kura 5,450 kwa asilimia 13 katika uchaguzi ulio wavutia jumla ya wagombea 9.
Wilson Mwaniki, wa chama cha Jubilee, ametangazua wa tatu kwa kura 198, akifuatwa na Stephen Wanyoike Waithaka wa chama cha National Liberation kwa kura 103, Kariuki Thimothy Kamau wa chama cha People Reinesence movement, akipata kura 51, Edwin Kariri Muchiri wa chama cha Party of National Unity, akipata kura 28. Naye Abudlahi Abdul Fatah wa chama cha Federal Party of Kenya akipata kura 19, Edward Mathenge Mwaniki wa chama cha Kenya Moja Movement, amepata kura 16, kisha Rachael Wangui Njoroge wa chama cha People’s Democratic akipata kura 11.
Akizungumza baada ya kutanzgazwa mshindi, Sammy Douglas Kamau Waweru, wa chama cha DCP, ameelezea furaha yake baada ya kushinda uchaguzi huo, na kuwapongeza wakaazi wa Ol Kalou walio simama naye katika uchaguzi huo, akiwashukuru kwa kutokubali kushawishiwa na wapinzani wao.
Vilevile amempongeza kinara wa chama chake cha DCP Rigathi Gachagua, kwa kumwaminia katika kinyang’anyiro hicho, na kumsaidia kufika hatua hiyo, pamoja na tume ya uchaguzi IEBC kwa kuendesha uchaguzi huo wa huru na haki.
Aidha amewataka wapinzani wake walioshindwa katika uchaguzi huo kuwa na moyo na kukubali matokeo.
Viongozi toka upande wa serikali na upinzani wamejitokeza kwa wingi na kumpongeza Sammy kwa kuibuka mshindi katika uchaguzi huo wa Ol Kalou.

