Mbunge wa Sigor, Peter Lochakapong’ amemtetea Waziri wa Afya, Aden Duale kufuatia madai ya kuchochea umma Kwa misingi ya kikabila, akisema kuwa matamshi yake yanawakilisha sauti na maslahi ya jamii za wafugaji nchini.
Akizungumza katika Kaunti ya Garissa, Lochakapong amesema kuwa Duale amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za jamii zilizotengwa kwa muda mrefu akihimiza usawa katika maendeleo na uwakilishi wa kisiasa.
Ameeleza kuwa viongozi kutoka maeneo ya wafugaji wana wajibu wa kuzungumza kwa sauti moja kuhusu changamoto zinazowakabili wananchi wao, ikiwemo huduma za afya, miundombinu na maendeleo.
Lochakapong amesisitiza kuwa kauli za Waziri Duale hazipaswi kutafsiriwa kisiasa, bali kama juhudi za kuangazia mahitaji ya wananchi wa maeneo ya wafugaji na kuhakikisha sauti yao inasikika katika maamuzi ya kitaifa.

