You are currently viewing MSAADA KWA WAKULIMA KUKABILIANA NA UKAME

MSAADA KWA WAKULIMA KUKABILIANA NA UKAME

Serikali imeanza kuweka mikakati ya kuwasaidia wakulima wanao kabiliwa na athari za ukame, uku hali ya ukame wa muda mrefu ukitishia uzalishaji wa mahindi katika baadhi ya maeneo nchini.

Waziri wa kilimo Mutahi Kagwe, amesema serikali itawasaidia wakulima walio athiriwa na mabadiliko ya tabia nchi, huku ikiweka mikakati ya kuhakikisha utosholezo wa chakula nchini.

Waziri Kagwe ameyasema hayo baadha ya kufanya ziara ya kutathmini hali ya kilimo katika kaunti za Uasin Gishu, Nandi na Trans-Nzoia, ambako amekiri kuwa hali mbaya ya anga imeathiri uzalishaji wa mahindi.

Waziri huyo sasa amewahakikishia wakenya kuwa taifa hili halitakabiliwa na uhaba wa chakula, licha ya changamoto zinazowakabili wakulima.

Aidha amesema serikali inaanda hatua za kuwalinda na kuwakinga wakulima dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, uku ikiimarisha uzalishaji wa chakula na kuhakikisha bidhaa muhimu zinapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu.

Waziri Kagwe pia ameonya kuhusu biashara ya mbegu gushi, akisema biashara hiyo haramu inadhoofisha uzalishaji wa chakula na kuwasababishia wakulima hasara kubwa.

Amesema kuwa baadhi ya wakulima ugundua kuwa walinunua mbegu bandia baada ya miezi mitano hadi sita, wakati mimea yao inaposhindua kuzaa.

Kagwe sasa amezitaka idara za usalama kuongeza msako dhidi ya wafanyibiashara wanao uza mbegu bandia, vilevile akiwataka wabunge kuunga mkono sheria itakayoweka uuzaji wa mbegu bandia kama uhalifu wa kiuchumi.

                                                                                                                                 APERIT FM HII NI YETU